JUKUMU LA VIJANA KATIKA KUFUFUA UCHUMI WA NCHI.


 
Vijana katika nchi ya Kenya wanalojukumu kubwa mno la kufufua na kukuza  uchumi wa nchi. Wanasema kwamba vijana ndio viongozi wa kesho. Pasipo kuwepo kwa vijana basi taifa lipo kwenye mtego ambao halitoweza kujinasua kesho.

Kila uchao, uchumi wa taifa unazidi kuzorota. Bei ya bidhaa inazidi kupanda na kumkandamiza mwananchi wa kawaida. Lakini vijana wana uwezo, ndio wana uwezo wa kubadili hali.

Idadi ya vijana ni kubwa sana hapa nchini Kenya. Wapo vijana wanaohitimu kila mwaka kutoka vyuo vikuu. Wapo wanaojihusisha na kazi za  jua kali ambapo wanafanya ufundi mbali mbali, wapo wanaojihusisha na ukulima  pamoja na mengine mengi.



Miezi michache iliopita, serikali ya Rais Ruto iliahidi kusambaza mbolea kwa wakulima nchini ili wakuze chakula na ili baadae uchumi wa taifa uweze kurejea katika Hali ya awali.

Vijana wanaojihusisha na ukulima walifaidika na mradi huu ambapo baadae serikali itawanunulia bidhaa zao na kupitia mazoa watakayo kua wamekuza, bei za bidhaa zitaweza kupungua.


Vijana pia wanajihusisha na ufundi mbali mbali na kazi tofauti za mikono. Na kupitia kazi hizi, vijana wataweza kufaidika kwa mradi mwengine wa serikali wa ujenzi wa nyumba. Maelfu ya vijana watapata ajira na kupitia nafasi zile za ajira, wataweza kuchangia kwenye ulipaji wa kodi, jambo ambalo litachangia kufufua naa kukuza uchumi wa taifa. 


Wengi wa vijana wamekua wakiishi na ukosefu wa kazi na kwa njia moja ama nyengine waliweza kuchangia kuzorota kwa uchumi wa nchi, kisa na maana wengi wao hawakua na kazi na kwa hivo ilikua ni changamoto kubwa sana kwao kuweza kulipa kodi. Lakini wapatapo ajira, wataweza kujikimu kimaisha, kulipakodi na kukuza uchumi wa taifa.



Halikadhalika, wapo vijana wanaohitimu kila uchao kwenye vyuo vikuu. Tumewaona vijana walio na ubunifu wa Hali ya juu. Tumeshuhudia wengine walio na vipaji ambavyo vimewawezesha kuwaajiri hata na vijana wenzoa. Hii inachangia ukuzaji wa uchumi, kwani wao na wale waliowaajiri wanakua kwenye nafasi ya kuweza kujitegemea na kulipa ushuru kwa nchi. Hii ama kwa hakika, inachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi/taifa.


                                               By Steve Kinyanjui 

Comments

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Endelea kutupa motisha na moyo wa kujihusisha na kilimo sisi kama vijana. Good job

    ReplyDelete

Post a Comment