MAKOVU YATAKAYODUMU MILELE.



 Jumapili ya tarehe 14 Juni 2014, ni tarehe iliyojaa kumbukumbu za jamaa ndugu na marafiki, waliopoteza maisha yao huko Mpeketoni kaunti ya Lamu, kwenye mashambukizi ya kigaidi.

Jumapili hii, kama siku zingine, wakazi wa Mpeketoni waliamka na kuanza shughuli zao za asubui kabla ya kwelekea kanisani, wasijue kilichowasubiri usiku ule. Hasara ya mali ya fedha nyingi, kulala kwa baridi na baya zaidi, kuwapoteza wapendwa wao.

Kwa hakika, jambo usilolijua nikama usiku wa kiza. Laiti wangejua walichopangiwa usiku ule, kwani wangenusuru maisha ya wengi waliouawa na kuwacha familia zao zikitaabika. Watoto waliachwa yatima, kina mama wakasalia wajane, kwa makosa wasiokuwanayo baba na waume zao. Majeraha walio nayo moyoni, yamesalia kuwa makovu, yasiosahaulika.

Ilikua ni mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni, wakati kundi la watu arubaini walioshukiwa kuwa kundi la wanamgambo wa Al-shabab waliingia mji wa Mpeketoni. Kundi hili, lilitumia magari matatu, mawili yakiwa aina ya 'Nissan' huku moja likiwa aina ya 'pick-up.'



Majambazi hao walikita kambi kando ya mji huo, huku wananchi wakiwaona ila wasijue wala kushuku kwamba walikua Majambazi.

Ilipowadia mwendo wa saa mbili unusu usiku, majambazi hao walijitawanya katika vikundi vikwili, ambapo kundi la kwanza liliingia nyumba kwa nyumba likitekeleza mauaji, huku kundi la pili likiwafyatulia risasi wakazi waliokua wakitembea na wengine waliokua wakitazama mpira wa Dunia (World Cup). Nyumba na magari pia hazikusazwa, kwani waliziteketeza bila kujali. 

Zaidi ya watu 60 walipoteza maisha yao, huku idadi kubwa ikiwa jamii ya wakikuyu. Chakusikitisha zaidi ni kwamba, wote waliouawa usiku ule walikua ni wanaume na wakristo. 

Baada ya kutekeleza mauaji hayo, wanamgambo hao wa Al-shabab waliyachoma magari yote matatu waliosafiria, na kutokomea kwenye msitu wa Boni. 

Mungu azidi kuzilaza roho za waliotuwacha mahali pema peponi. 


                                               By Steve Kinyanjui 


Comments

  1. Heko, ijapokuwa nasisitiza ujifunze kuwa mhariri wa kazi yako kabla ya kuichapisha.

    ReplyDelete
  2. sad story but niece one...good job

    ReplyDelete
  3. Kazi safi bro, unatukumbusha ndugu zetu walioangamia katika shambulizi Hilo na kamwe hatutalisahau.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Indeed hatutosahau. Mungu azidi kuzilaza roho zao mahala pema peponi.

      Delete
  4. We will always remember them😭 nice work my brother

    ReplyDelete
  5. So sad...RIP to all the souls we lost

    ReplyDelete
  6. Replies
    1. Kamwe halitotutoka ila kwa uwezo wa Mwenyezi Inshalaah

      Delete

Post a Comment