CHOZI LA PENZI.
Jina penzi litajwapo, kila mmoja hupiga taswira ya kile alichopitia ndani yake. Wengi wanapenda kwa maana hawajatendwa, wengine wanahofu, yasirejelee yaliowakuta awali na bado wapo wasio na Imani tena, kwa maana walishatendwa, wakalizwa, wakajeruhiwa na kuachiwa majeraha yasiyopona, na kwa wale waliopona, waliachwa na alama, alama ziishizo kuwapa kumbukumbu za awali milele.
Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Lakini, watayaganga vipi wakati nyoyo zilishalemaa? Wakati picha za akili, daima zinawapa kumbukumbu ya kusalitiwa, kudharauliwa na kutodhaminiwa na watu walio ishi kesema 'nakupenda' na kamwe sijapata kama wewe?
Inauma. Lakini, hivi Mapenzi ninini? Mbona upende leo na kesho uchukie? Mbona usifu leo na kesho ukashifu? Mbona? Ama kwakweli, huu ndio mtindo wa mapenzi unaotumika na kupatikana ndani ya vyuo vikuu. Sisemi kwamba nje watu wanapendana asilimia 100, la hasha! Tumeshuhudia nyingi za ndoa zikisambaratika, kisa na maana 'mpango wa kando'. Wanasema ukistaajabu ya Musa, utaona ya Firauni. Mengi ya tunayoyashuhudia nje, chanzo ni mtindo wa mahusiano uliopo ndani ya vyuo vikuu.
Ni mara ngapi tumesikia au hata kushuhudia watu wakijitia vitanzi, chanzo mapenzi? Hii ni dhahiri kwamba wapo watu walio na mapenzi ya dhati, lakini wanakosa wakuwapenda kwa dhati kama wapendavyo wao. Hizi ni nafsi na nyoyo ambazo baadae zinakosa Imani tena na penzi na hata kuishi maisha ambayo hawakukusudia au kutamani. Yaani mtu anapenda kwa dhati, anajitolea kwa Hali na Mali lakini mwisho wake anasalitiwa na mpenziwe, anavunjwa moyo, analizwa, anadunishwa kiasi cha kutoona dhamani yake tena. Hapa ndipo visa vya kujitia kitanzi au hata kumtia kitanzi mpenziwe zinachipukia. Upendo na Utu uliokuwa ndani ya mtu huyu mwaminifu, unamtoka na kuingia unyama, kutojali na mtu anakata kauli ya kuishi atakavyo, kutopenda tena au hata kuandaa visasi. Watu wazuri wanabadilika huku idadi ya wazuri ikizidi kudidimia. Huenda waliosalia, wanahesabika.
Vyuo vikuu vimekua ni vyanzo vya haya yote. Nafsi nzuri zakupendeza na kutamanika, zimeishia kaburini, huku zingine zikibadilika, ili zilipize visasi. Kinachouma na kinachosikitisha mno ni kwamba, visasi hivi vinalipizwa kwa nafsi zingine zisizonahatia, tena nafsi nzuri ambazo baadae zinaishia kaburini au kubadilika na kuwa mbaya hata zaidi.
Je, ni nani ata zungumza na nafsi hizi zilizoko ndani ya vyuo vikuu, ili vizazi vingine vijavyo viwe kama wazazi wetu? Vikundi vibaya vya marafiki, vinazidi kupotosha nafsi njema na hivyo kesho, huenda kukawa kubaya hata zaidi.
Kaburi imewameza wengi, tena wasio na hatia. Hatia kubwa walio fanya, ni kupenda kwa dhati. Miji na vijiji vimejaa watu waliotendwa, wasio penda na wakipenda basi hawapendi kwa Mapenzi bali kwa mali wafaidikayo kwayo.
Lakini ni na Imani, kuwa kizazi kilichoko ndani ya vyuo vikuu, kikipenda kwa dhati, kirejeshe uaminifu, kidhamini mahusiano, basi kesho kutakua na mwanga, ndani ya marafiki, wapenzi, wanandoa na familia kwa ujumla. Inawezekana.
By Steve Kinyanjui.
Good job
ReplyDeleteMapenzi. Kumpenda mtu Kisha kumchukia ni jambo ambalo halitawahi eleweka. I will never leave you to cheating.Mungu na atusaidie
ReplyDeleteπ
DeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteπ€
Deletepenzi kipofu eti ukipenda kwama kujikwamua ni wewe kuamua...tufunguke macho tujilinde na makovu ya mapenzi
ReplyDeleteπ€
DeleteHongera kazi nzuri
ReplyDeleteπ€
DeleteNice article π
ReplyDeleteπ€
DeleteKazi safi
ReplyDeleteπ€
DeleteNakala nzuri sana
ReplyDeleteπ€
DeleteNakala safi
ReplyDeleteπ€
DeleteSafiiii
ReplyDeleteπ€
DeleteNice
ReplyDeleteπ€
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteKweli kabisaa π―
ReplyDeleteπ€
DeleteHeko Kwa kazi nzuri π₯π₯
ReplyDeleteπ€
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteπ€
DeleteKweli kabisa
ReplyDeleteIla mara nyengine unatakiwa kuwa mbinafsi ili kujiepusha na majinamizi ya mapenzi.
Kazi safi kaka
π€
DeleteKazi safii
ReplyDeleteπ€
DeleteNice one bro
ReplyDeleteπ€
DeleteKweli kabisa , napenda kazi nzurii hii
ReplyDeleteπ€
DeleteKazi safii
ReplyDeleteπ€
DeleteNice content
ReplyDeleteπ€
DeleteNzuri kabisa ,,,huh unapenda Leo kesho wachukia weuh
ReplyDeleteπ€
DeleteKazi safi
ReplyDeleteπ€
DeleteMakala safi kaka
ReplyDeleteπ€
DeleteNice article π
ReplyDeleteKazi safi sana bro
ReplyDeleteKazi kuntuπ
ReplyDeleteHeko ππΏ
ReplyDeleteWord✅
ReplyDeleteπ€
DeleteUmegonga msumari Moto juu ya kidonda ,kaz yako iko kuntu
ReplyDeleteNakala safi sana ya kiswahili. Inatuelimisha kuhusu Mapenzi
ReplyDeleteSafi sana
ReplyDeleteChozi jamani latirika kwa wengiπ₯π₯π₯
ReplyDeleteKazi safii
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteShwari my guy
ReplyDeleteChozi la mnyonge
ReplyDeleteNyc bro
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice one π₯π₯
ReplyDelete