ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA.

 


Mabadiliko ya Hali ya hewa yameshuhudiwa katika nchi tofauti Duniani ambapo mimea, wanyama na binadamu wameadhirika na wengine hata kufariki dunia. Hata hivyo, Kenya haijasazwa, kwani tumeshuhudia baadhi ya maeneo nchini yakiadhirika kwa ukame ambapo mimea imenyauka, wanyama nao sawia na binadamu wakidhoofika na kufariki, yote kwaajili ya ukosefu wa maji/mvua.

Ni juzi tu ambapo takriban Kaunti thelathini zimeripotiwa kuadhirika kwa ukame na kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba maeneo haya yanasaidiwa kwa kupewa msaada wa  chakula.

Hii ni baadhi ya madhara yaletwayo na mabadiliko ya Hali ya hewa. Ukosefu wa mvua husebabisha ukame ambapo viumbe wengi, wanyama kwa binadamu sawia na mimea huadhirika pakubwa. 



Waswahili husema kwamba maji ni uhai, hii imedhihirika dhahiri siku chache, wakati wakazi wa Kaunti ya Baringo walionekana wakichimba mto uliokauka ili angalau wapate tone la maji. Baya zaidi ni kwamba maji waliotafuta kwa udi na uvumba yalikua ni maji machafu ajabu, ingawaje walionekana wakiyanywa kwa kukosa mbinu mbadala. 

Hata hivyo, zipo baadhi ya sababu zanazochangia mabadiliko ya Hali ya hewa. Moja wapo ya sababu hizi, ni ukataji wa miti kiholela bila upanzi wa mingine. Wakati watu wanajitahidi kukata miti, ndivyo wanavyozidi kujiweka kwenye hatari ya kukumbwa na ukame. 



Mimea inayopandwa ili kuleta mazao nayo hushindwa kustahimili mahali ya jua na ukosefu wa mvua. Hii huchangia kunyauka kwa mimea Ile. Upande mwengine, mazao yakosekanapo njaa hubisha hodi nayo mvua ikosekanapo ukame huingia. 

Mabadiliko ya Hali ya hewa vilevile husebabisha kudhorota kwa uchumi wa nchi. Nchi ya Kenya hutegemea kwa kiwango kikubwa ukulima wa chakula. Huu ndio uti wa mgongo wa nchi hii. Hivyo basi, ukame uingiapo basi uzalishaji wa chakula hupungua na kusebabisha kudhorota kwa uchumi wa nchi. 

Hata hivyo itakua jambo la busara zaidi iwapo wakenya watajitahidi kwenye upanzi wa miti na kukomesha ukataji wa miti au misitu. Kwa hatua hii, tutaweza kukabiliana na janga la ukame. 


                                         By Steve Kinyanjui 

Comments

  1. Mabadiliko ya tabia nchi ilekuwa swala kuu Sasa. Serikali inapaswa kubalili mienendo.
    Kazi nzuri

    ReplyDelete
  2. Kweli mabadiliko yana athari nyingi mno

    ReplyDelete
  3. Kazi nzuri kaka. Endelea kutuelimisha kuhusu mazingira yetu.

    ReplyDelete
  4. Kazi safi mkuu๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete

Post a Comment