TUM YANILETEA UHALISIA WA NDOTO.
Mara nyingi watoto huwa na maono ya kuwa mtu au kitu fulani katika maisha. Jambo ambalo hukuzwa zaidi na mzazi au hata mwalimu pale shuleni. Ndiposa utamsikia mzazi au mwalimu akimuuliza mtoto angependa kuwa nani awapo mtu mzima. Ni jambo ambalo humwezesha mtoto kufahamu kwamba anao uwezo na nafasi ya kipekee kuwa yeyote atakaye maishani, bora bidii na imani. Kama iwafanyikiavyo watoto wengine, haikua tofauti kwangu. Awali katika umri wangu mdogo, nilitamani sana kuwa daktari, wala si daktari tu bali daktari wa upasuaji. Hili lilitokana na kuwasikiliza watoto wenzangu waliotamani kuwa madaktari, nami nikawaiga. Sikutambua kwamba kila mtu aliumbwa na utofauti wa kipekee na kwamba maishani tungekuwa watu sawa lakini wanaojihusisha na mambo tofauti, nazungumzia wapo wangekua madaktari, walimu, wanahabari na mengineyo. Jambo hili la mimi kuwa daktari liliendelea hadi nilipokuwa katika shule ya upili. Ndipo tulizungumziwa nikiwa kidoto cha pili wakati wa kuchagua masomo manane ambayo ...