ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA.
Mabadiliko ya Hali ya hewa yameshuhudiwa katika nchi tofauti Duniani ambapo mimea, wanyama na binadamu wameadhirika na wengine hata kufariki dunia. Hata hivyo, Kenya haijasazwa, kwani tumeshuhudia baadhi ya maeneo nchini yakiadhirika kwa ukame ambapo mimea imenyauka, wanyama nao sawia na binadamu wakidhoofika na kufariki, yote kwaajili ya ukosefu wa maji/mvua. Ni juzi tu ambapo takriban Kaunti thelathini zimeripotiwa kuadhirika kwa ukame na kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba maeneo haya yanasaidiwa kwa kupewa msaada wa chakula. Hii ni baadhi ya madhara yaletwayo na mabadiliko ya Hali ya hewa. Ukosefu wa mvua husebabisha ukame ambapo viumbe wengi, wanyama kwa binadamu sawia na mimea huadhirika pakubwa. Waswahili husema kwamba maji ni uhai, hii imedhihirika dhahiri siku chache, wakati wakazi wa Kaunti ya Baringo walionekana wakichimba mto uliokauka ili angalau wapate tone la maji. Baya zaidi ni kwamba maji waliotafuta kwa udi na uvumba yalikua ni maji machafu ...