MAKOVU YATAKAYODUMU MILELE.
Jumapili ya tarehe 14 Juni 2014, ni tarehe iliyojaa kumbukumbu za jamaa ndugu na marafiki, waliopoteza maisha yao huko Mpeketoni kaunti ya Lamu, kwenye mashambukizi ya kigaidi. Jumapili hii, kama siku zingine, wakazi wa Mpeketoni waliamka na kuanza shughuli zao za asubui kabla ya kwelekea kanisani, wasijue kilichowasubiri usiku ule. Hasara ya mali ya fedha nyingi, kulala kwa baridi na baya zaidi, kuwapoteza wapendwa wao. Kwa hakika, jambo usilolijua nikama usiku wa kiza. Laiti wangejua walichopangiwa usiku ule, kwani wangenusuru maisha ya wengi waliouawa na kuwacha familia zao zikitaabika. Watoto waliachwa yatima, kina mama wakasalia wajane, kwa makosa wasiokuwanayo baba na waume zao. Majeraha walio nayo moyoni, yamesalia kuwa makovu, yasiosahaulika. Ilikua ni mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni, wakati kundi la watu arubaini walioshukiwa kuwa kundi la wanamgambo wa Al-shabab waliingia mji wa Mpeketoni. Kundi hili, lilitumia magari matatu, mawili yakiwa aina ya 'Nissan' hu...