Posts

TUM YANILETEA UHALISIA WA NDOTO.

Image
  Mara nyingi watoto huwa na maono ya kuwa mtu au kitu fulani katika maisha. Jambo ambalo hukuzwa zaidi na mzazi au hata mwalimu pale shuleni. Ndiposa utamsikia mzazi au mwalimu akimuuliza mtoto angependa kuwa nani awapo mtu mzima. Ni jambo ambalo humwezesha mtoto kufahamu kwamba anao uwezo na nafasi ya kipekee kuwa yeyote atakaye maishani, bora bidii na imani. Kama iwafanyikiavyo watoto wengine, haikua tofauti kwangu. Awali katika umri wangu mdogo, nilitamani sana kuwa daktari, wala si daktari tu bali daktari wa upasuaji. Hili lilitokana na kuwasikiliza watoto wenzangu waliotamani kuwa madaktari, nami nikawaiga. Sikutambua kwamba kila mtu aliumbwa na utofauti wa kipekee na kwamba maishani tungekuwa watu sawa lakini wanaojihusisha na mambo tofauti, nazungumzia wapo wangekua madaktari, walimu, wanahabari na mengineyo. Jambo hili la mimi kuwa daktari liliendelea hadi nilipokuwa katika shule ya upili. Ndipo tulizungumziwa nikiwa kidoto cha pili wakati wa kuchagua masomo manane ambayo ...

JUKUMU LA VIJANA KATIKA KUFUFUA UCHUMI WA NCHI.

Image
  Vijana katika nchi ya Kenya wanalojukumu kubwa mno la kufufua na kukuza  uchumi wa nchi. Wanasema kwamba vijana ndio viongozi wa kesho. Pasipo kuwepo kwa vijana basi taifa lipo kwenye mtego ambao halitoweza kujinasua kesho. Kila uchao, uchumi wa taifa unazidi kuzorota. Bei ya bidhaa inazidi kupanda na kumkandamiza mwananchi wa kawaida. Lakini vijana wana uwezo, ndio wana uwezo wa kubadili hali. Idadi ya vijana ni kubwa sana hapa nchini Kenya. Wapo vijana wanaohitimu kila mwaka kutoka vyuo vikuu. Wapo wanaojihusisha na kazi za  jua kali ambapo wanafanya ufundi mbali mbali, wapo wanaojihusisha na ukulima  pamoja na mengine mengi. Miezi michache iliopita, serikali ya Rais Ruto iliahidi kusambaza mbolea kwa wakulima nchini ili wakuze chakula na ili baadae uchumi wa taifa uweze kurejea katika Hali ya awali. Vijana wanaojihusisha na ukulima walifaidika na mradi huu ambapo baadae serikali itawanunulia bidhaa zao na kupitia mazoa watakayo kua wamekuza, bei za bidhaa zitawe...

ATHARI ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA.

Image
  Mabadiliko ya Hali ya hewa yameshuhudiwa katika nchi tofauti Duniani ambapo mimea, wanyama na binadamu wameadhirika na wengine hata kufariki dunia. Hata hivyo, Kenya haijasazwa, kwani tumeshuhudia baadhi ya maeneo nchini yakiadhirika kwa ukame ambapo mimea imenyauka, wanyama nao sawia na binadamu wakidhoofika na kufariki, yote kwaajili ya ukosefu wa maji/mvua. Ni juzi tu ambapo takriban Kaunti thelathini zimeripotiwa kuadhirika kwa ukame na kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba maeneo haya yanasaidiwa kwa kupewa msaada wa  chakula. Hii ni baadhi ya madhara yaletwayo na mabadiliko ya Hali ya hewa. Ukosefu wa mvua husebabisha ukame ambapo viumbe wengi, wanyama kwa binadamu sawia na mimea huadhirika pakubwa.  Waswahili husema kwamba maji ni uhai, hii imedhihirika dhahiri siku chache, wakati wakazi wa Kaunti ya Baringo walionekana wakichimba mto uliokauka ili angalau wapate tone la maji. Baya zaidi ni kwamba maji waliotafuta kwa udi na uvumba yalikua ni maji machafu ...

FURAHA JIJI LA MOMBASA OPERESHENI ZA BANDARI ZIKIREJESHWA PWANI.

Image
   Waswahili husema, siku njema huonekana asubui. Tarehe 13/9/2022, ndio iliyokua tarehe ya kumwapisha Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya, Daktari William Samoei Ruto na naibu wake Bw. Rigathi Gachagua. Hii ilitokea tu baada ya Wakenya kushiriki kwenye uchaguzi wa Agosti 9,2022 ambapo William Ruto alitangazwa mshindi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kupitia kwa Mwenye kiti wake Bw. Wafula Chebukati. Awali kabla ya uchaguzi, Kaunti ya Mombasa ilitambulika kuwa ngome ya mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya unaoongozwa na Raila Odinga. Baadae hii ilidhihirika baada ya uchaguzi, kwani Raila Odinga alizoa kura nyingi zaidi ya mpinzani wake William Ruto.  Wakazi wa Mombasa wakighadhabishwa na ushindi wake William Ruto, waaliamini kwamba wangesahaulika kwenye serikali Ile, wasijue mpango aliokua nao William Ruto kwao.  Siku ya Kuapishwa kwake kama Rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya, Rais Ruto aliwashangaza wengi kwenye hotuba yake, alipoahidi kurejesha operesheni za ban...

CHOZI LA PENZI.

Image
  Jina penzi litajwapo, kila mmoja hupiga taswira ya kile alichopitia ndani yake. Wengi wanapenda kwa maana hawajatendwa, wengine wanahofu, yasirejelee yaliowakuta awali na bado wapo wasio na Imani tena, kwa maana walishatendwa, wakalizwa, wakajeruhiwa na kuachiwa majeraha yasiyopona, na kwa wale waliopona, waliachwa na alama, alama ziishizo kuwapa kumbukumbu za awali milele. Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Lakini, watayaganga vipi wakati nyoyo zilishalemaa? Wakati picha za akili, daima zinawapa kumbukumbu ya kusalitiwa, kudharauliwa na kutodhaminiwa na watu walio ishi kesema 'nakupenda' na kamwe sijapata kama wewe?  Inauma. Lakini, hivi Mapenzi ninini? Mbona upende leo na kesho uchukie? Mbona usifu leo na kesho ukashifu? Mbona? Ama kwakweli, huu ndio mtindo wa mapenzi unaotumika na kupatikana ndani ya vyuo vikuu. Sisemi kwamba nje watu wanapendana asilimia 100, la hasha! Tumeshuhudia nyingi za ndoa zikisambaratika, kisa na maana 'mpango wa kando...

MAKOVU YATAKAYODUMU MILELE.

Image
 Jumapili ya tarehe 14 Juni 2014, ni tarehe iliyojaa kumbukumbu za jamaa ndugu na marafiki, waliopoteza maisha yao huko Mpeketoni kaunti ya Lamu, kwenye mashambukizi ya kigaidi. Jumapili hii, kama siku zingine, wakazi wa Mpeketoni waliamka na kuanza shughuli zao za asubui kabla ya kwelekea kanisani, wasijue kilichowasubiri usiku ule. Hasara ya mali ya fedha nyingi, kulala kwa baridi na baya zaidi, kuwapoteza wapendwa wao. Kwa hakika, jambo usilolijua nikama usiku wa kiza. Laiti wangejua walichopangiwa usiku ule, kwani wangenusuru maisha ya wengi waliouawa na kuwacha familia zao zikitaabika. Watoto waliachwa yatima, kina mama wakasalia wajane, kwa makosa wasiokuwanayo baba na waume zao. Majeraha walio nayo moyoni, yamesalia kuwa makovu, yasiosahaulika. Ilikua ni mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni, wakati kundi la watu arubaini walioshukiwa kuwa kundi la wanamgambo wa Al-shabab waliingia mji wa Mpeketoni. Kundi hili, lilitumia magari matatu, mawili yakiwa aina ya 'Nissan' hu...